KESHO HAiFIKI

6c029a25eb3a4b2cec25f37b312ead03--il-corvo-raven-art
Viongozi kesho,inafaa kutupiliwa mbali,
Kuwapa kipaumbele,kuwazindua katika ajira,
Jana leo,na bado hawajangatuka,
Sekta zote,kuwapa matumaini maisha,
Jinsi itaamuliwa,sera kuwahusu itakavyobuniwa,
kutamauka huku,huwafanya kujiusisha uraibu,
Hatima miongoni,miongoni vitendo vingine,
Watapata afueni,sana humu nchini,

Daima naondoka,siwati kukumbuka popote,
Siku moja,lazima tutakutana mwandani,
Tuwe hai,kwa hili nina yakini,
Ningaliruka nawe,lau ningekuwa na bawa,
Nakumbuka nasikitika,nawe mbali tungawa,
Kaa ukijua,simanzi moyoni mwangu,
Heri kuwaona,pamoja takuja kuwa,
Nawe sitahimili,hili kaa ukijua.

One thought on “KESHO HAiFIKI

Comments are closed.